Habari kutoka nchini Yemen zinaeleza kuwa mapigano makali yamepamba moto
katika mji mkuu wa nchi hiyo wakati ambapo wanamgambo wa Kishia wa
Huthi wakijaribu kuuteka Ikulu ya nchi hiyo.
Mapigano
hayo yalikuja wakati ambapo wanamgmbo wa Huthi walipofanya mashambulio
ya kupangwa dhidi ya kikosi cha Haraasul Jamhuri wanaolinda Ikulu ya
Rais wa nchi hiyo.
Waandishi wa habari waliripoti jana kuwa makali ya
mapigano yaliendelea kusini mwa mji wa San'aan na pembezoni mwa Majengo
ya Kasri ya Ikulu wa Rais Abdi Rabih Hadi Mansuri kiongozi wa Utawala
Kibaraka wa Yemen.
Habari
zaidi zinaeleza kuwa wanamgambo wa Kishia wa Yemen wanajaribu kuuchukua
Ikulu ya nchi hiyo siku mbili zilizopita walimteka Mkurugenzi wa
Ikulu,na inaaminika wanasonga pole pole kuelekea Ikulu.
Mwezi september mwaka jana wanamgambo hao walio mawakala wa Iran waliutwaa mji wa San'aa na maeneo mengi ya miji muhimu nchini Yemen.
0 comments:
Post a Comment