Rais Barack Obama wa Marekani amesisitiza kwamba Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran imetekeleza kikamilifu ahadi zake kwenye makubaliano ya
nyuklia na kuongeza kuwa, ataupigia kura ya veto mpango wowote
utakaowasilishwa kwenye Baraza la Kongresi la nchi hiyo wenye shabaha ya
kuvuruga mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1.
Akizungumza na kanali ya televisheni ya CNN, Rais Obama ameongeza kuwa,
Iran imetekeleza kikamilifu ahadi ilizozitoa kwenye makubaliano ya muda
ya nyuklia na kusisitiza kwamba pande hizo mbili zina fursa ya kufikia
makubaliano ya mwisho. Rais wa Marekani ameelezea changamoto anazoweza
kukabiliana na mrengo wa Republican kwenye kongresi kuhusiana na miradi
ya nyuklia ya Iran inayaotekelezwa kwa malengo ya amani na kusisitiza
kwamba, jambo lililo na umuhimu ni kufikiwa makubaliano ya mwisho.
Kuhusiana na mpango wa John Boehner Spika wa Kongresi ya Marekani wa
kutaka kumualika Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel na ahutubie
kwenye kongresi, Rais Obama amebainisha kwamba hatakutana na Netanyahu
kwenye safari yake ya Washington. Inafaa kuashiria hapa kuwa, mrengo wa
Republican wenye viti vingi kwenye kongresi, unafanya njama za kuvuruga
mwenendeo wa mazungumzo ya nyuklia kutokana na mashinikizo ya Lobi ya
Wazayuni. Mrengohuo pia unataka kupitisha vikwazo vipya dhidi ya Iran,
suala ambalo limekabiliwa na radiamali kali ya Obama na viongozi wengine
wa White House.
0 comments:
Post a Comment