Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Tawi la Afrika Kusini inamsaka aliyekuwa katibu wake, (jina
linahifadhiwa), ili kimfikisha katika vyombo vya kisheria, kutokana na
tuhuma za utapeli.
Anatuhumiwa kuwatapeli baadhi ya Watanzania
waishio Afrika Kusini, Rand 200,000, zaidi ya Sh37 milioni, kwa kutumia
kampuni iliyosajiliwa kwa jina la mkewe, ya masuala ya Teknolojia ya
Mawasiliano.
Anadaiwa kuwa alifanikiwa kuwatapeli Watanzania
hao kiasi hicho cha pesa kwa mtindo wa upatu, baada ya kuwashawishi
wawekeze pesa zao katika kampuni hiyo na kwamba baada ya muda wangepata
faida.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa alifanikiwa
kuwashawishi Watanzania hao kuwekeza pesa zao katika kampuni hiyo akidai
kuwa ilikuwa inashughuli za biashara ya (Forex & Stock Marketing),
lakini baada ya Watanzania hao kuwekeza, alikimbia nazo bila kuwalipa.
Mwenyekiti wa CCM Tawi la Afrika Kusini, Kelvin
Nyamori alilithibitishia Mwananchi na kusema kuwa kutokana na tuhuma
hizo aliitisha kikao cha dharura cha Sekretarieti na kumvua wadhifa wake
huo na kutoa taarifa katika mamlaka mbalimbali vikiwamo vyombo vya
kisheria.
“Kamati, tulishafanya kikao cha dharura
kumsimamisha kazi yake ya ukatibu, baada ya kupata tarifa hizo, kutokana
na malalamiko ya waliodhulumiwa,” alisema Nyamori na kuongeza:
“Tumeshatoa taarifa Ubalozini na kituo cha polisi.
Tunamtafuta mtuhumiwa ili tumfikishe kwenye vyombo vya sheria, kwa
kufanya utapeli kwa kutumia jina la chama kimya kimya.
Alitoa wito kwa mtu yeyote Tanzania anayemfahamu,
atakapomuona au kama anajua mahali aliko, atoe ushirikiano kwa
kuwasiliana na CCM Afrika Kusini.
chanzo mwananchi
0 comments:
Post a Comment