kikosi cha zima moto kikifanya kazi yake hospitalini TMJ

Wagonjwa wakitolewa nje na manesi wa Hospital ya TMJ baada ya kuwaka moto muda mfupi uliopita.
Hospital ya TMJ iliyopo Mikocheni Dar es salaam inawaka moto hivi
sasa. Kwa mujibu wa taarifa za mashuhuda waliyopo eneo la tukio, moto…
Baadhi ya wagonjwa wakiwa wametolewa hospitali ya TMJ baada ya nyumba ya jirani kuwaka moto. Walitolewa wodini kwa tahadhari.
Mgonjwa alitolewa nje ya wodi na jamaa yake.
Mhudumu akimtoa nje ya wodi mgonjwa, kwa tahadhari baada ya nyumba jirani na hospitali hiyo kuwaka moto.

Kikosi cha Kuzima Moto kikizima moto nyumba jirani na Hospital ya
TMJ iliyopo Mikocheni Dar es Salaam muda huu na watu kudhani kuwa
iliyokuwa ikiungua ni hospitali.

Wagonjwa wakitolewa nje na manesi wa Hospital ya TMJ baada ya nyumba jirani kuwaka moto.
Hospital ya TMJ iliyopo Mikocheni Dar es Salaam ilizushiwa kuwaka
moto baada ya nyumba jirani kulipuka moto, hali iliyosababisha hekaheka
kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo ya kuwatoa nje wagonjwa kwa tahadhari.
Tahadhari hiyo ilichukuliwa kutokana na wasiwasi kuwa moto huo
ungeweza kuvuka na kuingia hospitali lakini ulidhibitiwa na kikosi cha
zima moto na kuishia katika nyumba hiyo ya jirani.
0 comments:
Post a Comment