Na Shemsia
Khamis, PEMBA
MAHAKAMA ya
Mkoa Chakechake, chini ya Hakimu Khamis Ramadhan Abdalla, imempandisha
kizimbani mshtakiwa Abuu Said Omar (15), mkaazi wa Wawi Chakechake, kujibu
tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume (14), zilizomkabili mahakamani hapo.
Ilidaiwa mahakamani hapo, na Mwendeshamashtaka Ali Bilali Hassan
kuwa, mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo, Machi 14 mwaka huu majira ya saa 7:00
mchana.
Mwendeshamashtaka alidai kuwa, mshtakiwa bila halali alimuingilia
mtoto huyo kinyume na maumbile, katika mabonde ya Wawi mtegani, wilaya ya
Chakechake.
Baada ya mshtakiwa huyo, kusomewa shitaka lake, alikana na
kuiyomba mahakama impatie dhamana, kutokana na kuwa ni haki yake ya kisheria.
‘’Muheshimiwa Hakimu, naiyomba mahakama yako tukufu, inipatie
dhamana kutokana na kuwa, ni mwanafunzi wa darasa la sita, hivyo nikienda
rumande nitakosa kusoma’’, alidai mshtakiwa.
Kufuatia ombi hilo, Mwendesha mashtaka alidai hana pingamizi
yoyote endapo mshtakiwa ataweza kutimiza masharti ya dhamana atakayopewa na
mahakama.
Hakimu aliyataja masharti ya dhamana, kuwa ni pamoja na yeye
binafsi kujithamini shilingi milioni 2,000,000 za maandishi na wadhamini wawili,
kima kama hicho za maandishi.
‘’Mshtakiwa wathamini wako wawe na vitambulisho vya uzanzibar
ukaazi na barua za sheha katika shehia wanazoishi ndipo tuweze kukupa
dhamana’’, alisema Hakimu.
Baada ya mshtakiwa kuweza kutimiza masharti ya dhamana, bila ya
pingamizi yoyote mahakamani hapo, ndipo Hakimu alipomuamuru mshtakiwa kwenda
nje hadi siku hiyo.
Kwa mujibu wa sheria kufanya hivyo, ni kosa kinyume na kifungu cha
sheria cha 150 (a), sheria namba 6 ya mwaka 2004, sheria ya Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment