
Waziri mkuu nchini Mali Oumar
Tatamy Ly pamoja na baraza lake la mawaziri wamejiuzulu,miezi minane tu
baada ya demokrasia kurudi nchini humo kufuatia udhibiti wa eneo la
kazkazini uliotekelezwa na wanamgambo wa kiislamu.
Mabadiliko katika serikali yalitarajiwa
kufanyika ,lakini mwandishi wa BBC katika mji mkuu wa Mali
Bamako,anasema kuwa kiwango cha mabadiliko hayo hakikutarajiwa.Waziri mkuu mpya ,Moussa Mara amekuwa mpinzani mkuu wa rais Boubakr Keita hapo awali.
Bwana Mara aliye na umri wa miaka 39 amekuwa akiitaka serikali kuimarisha usalama katika eneo la kazkazini la nchi hiyo.
bbc
0 comments:
Post a Comment