pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

MFANYABIASHARA WA BUTCHER AMCHARANGA MAPANGA MFANYAKAZI WAKE

 

Sunday Mwambelo baada ya kucharangwa mapanga na bosi wake ndani ya buncha eneo la Sae Jijini Mbeya




Ndugu jamaa na marafiki wa Sunday Mwambelo wakimjulia hali katika hospitali ya rufaa Mbeya alikolazwa baada ya kucharangwa mapanga na bosi wake aliyefahamika kwa jina la Simon Njangaje 

Sunday Mwambelo akijuliwa hali na dada yake Never Mwambinga katika hospitali ya Rufaa Mbeya alikolazwa baada ya kucharangwa mapanga na bosi wake 



WAKAZI wa kitongoji cha Sae Jijini Mbeya hivi karibuni walimuokoa na kifo mfanyabiashara wa bucha katika buncha ya Simon Butchery iliyopo Sae Jijini Mbeya, Sunday Mwambelo ambaye alifungiwa katika bucha na kucharangwa mapanga na watu wawili waliofahamika kwa majina ya Simon Njangale na Daud Edson.

Hatua hiyo ilifuatia tukio la kutisha ambalo lilikuwa linaendelea katika moja ya vyumba vya bucha la nyama ambapo watu watatu walifika eneo hilo majira ya saa 1:00 jioni na kuufunga mlango wa bucha hiyo kwa nje kisha wakaanza kumcharaza mapanga muuza nyama huyo.

Ilidaiwa kuwa mara baada ya watu hao kuingia katika bucha hilo walizima mshumaa ambapo mmoja wao alibaki mlangoni na wawili kati yao waliingia buchani na kuchukua panga na shoka kisha kuanza kumuadhibu Sunday ambaye ndiye muuzaji wa nyama katika bucha hiyo.

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mmoja kati ya watu hao ndiye mmiliki wa bucha hiyo na kuwa walifikia hatua hiyo baada ya mfanyakazi wa buchani hapo kuingiza hasara ya sh.25,000 ambazo ni sehemu ya fedha za mauzo ya siku hiyo.

Kwa mujibu wa Mwambelo ambaye amedumu katika biashara hiyo kwa zaidi ya miaka 10 ni kwamba mara baada ya kuulizwa kuhusu hasara ya kiasi hicho cha fedha alimwambia tajiri yake kuwa atafidia hasara hiyo kesho yake jambo ambalo tajiri wake hakukubaliana nalo na hivyo kuchukua uamuzi wa kumkata kwa mapanga na kusababisha damu nyingi kumwagika buchani

0 comments:

Post a Comment