
Timu ya Taifa ya Watoto wa
Mitaani ya Tanzania imetwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani baada
ya kuilaza Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jana
(Aprili 6), jijini Rio de Janeiro, Brazil
Mshambuliaji Frank William alifunga
mabao matatu katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja mkongwe na maarufu wa
klabu ya Fluminense huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Fedha wa
Uingereza, George Osborne.
Tanzania ilipata tiketi ya kucheza
fainali baada ya kuitandika Marekani mabao 6-1 ambapo hadi mapumziko
ilikuwa mbele kwa mabao 4-0.
Burundi ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi ya nusu fainali ya pili.
Timu ya Tanzania inarejea nchini
Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.
0 comments:
Post a Comment